EconPapers    
Economics at your fingertips  
 

Taswira ya Jamii ya Kisasa kwa Mujibu wa Riwaya Teule za Kisasa za Mwandishi K.W. Wamitila

Janice M. Mutua ()

International Journal of Linguistics, 2022, vol. 3, issue 1, 1 - 19

Abstract: Lengo: Makala hii inakusudia kuangazia taswira kamili ya jamii ya kisasa kama ilivyodhihirika katika riwaya mpya teule za Musaleo! na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji zilizoandikwa na K.W. Wamitila. Mwandishi amefanikiwa kuieleza jamii ya kisasa kupitia kwa usimulizi wenye simulizi nyingi fupi fupi ambayo ni kipengee kimojawapo cha mbinu ya utunzi ya kimajaribio. Mbinu ya utafiti: Mtafiti aliafikia lengo la utafiti kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo mkabala wa ufasili. Mtafiti ameangazia maandiko yenye uhusiano na jinsi riwaya mpya ilivyoichorea hadhira taswira ya jamii husika. Kipengee cha kimajaribio kilichotumika ni matumizi ya simulizi fupi fupi zilizomo katika simulizi kuu. Data ya utafiti ilikusanywa maktabani kutoka katika uchambuzi wa maudhui katika riwaya za Musaleo! (ML) na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji (MMM). Nadharia ya Usasaleo kama ilivyoasisiwa na Jean Baudrillard iliuongoza utafiti katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Matokeo: Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa utaratibu katika utekelezaji wa shughuli mbali mbali uandishi ukiwemo, waweza kuonekana usiofaa lakini hiyo ndiyo taswira kamili ya maisha katika jamii ya kisasa; hayana utaratibu mahususi. Hali ya mparaganyiko imechukua nafasi kubwa ya maisha ya kisasa. Makala imebainisha kuwa jamii inakabiliana na changamoto nyingi. Aidha imeonyesha jinsi jamii yenyewe inavyojimudu kuzitatua. Mchango wa Kipekee kwa Mujibu wa Nadharia: Mintarafu ya nadharia, mwandishi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya zifuate utaratibu mahususi. Hii ni kwa sababu maisha katika jamii ya kisasa hayana utaratibu wowote.

Keywords: taswira ya kisasa; jamii ya kisasa; usasaleo; riwaya mpya (search for similar items in EconPapers)
Date: 2022
References: Add references at CitEc
Citations:

Downloads: (external link)
https://iprjb.org/journals/index.php/IJL/article/view/1538 (application/pdf)

Related works:
This item may be available elsewhere in EconPapers: Search for items with the same title.

Export reference: BibTeX RIS (EndNote, ProCite, RefMan) HTML/Text

Persistent link: https://EconPapers.repec.org/RePEc:bdu:ojtijl:v:3:y:2022:i:1:p:1-19:id:1538

Access Statistics for this article

More articles in International Journal of Linguistics from IPRJB
Bibliographic data for series maintained by Chief Editor ().

 
Page updated 2025-07-19
Handle: RePEc:bdu:ojtijl:v:3:y:2022:i:1:p:1-19:id:1538