MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIMU (MEMES) KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NCHINI KENYA
Anne Wangari Munuku ()
International Journal of Linguistics, 2022, vol. 3, issue 1, 30 - 49
Abstract:
Makala hii imeangazia lugha ya mawasiliano katika utanzu mpya wa mimu ambao ni aina ya fasihi kidijitali katika mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp nchini Kenya. Matlaba ya makala hii ni kufafanua utanzu huu katika muktadha wa matumizi ya lugha nchini Kenya. Uundaji mimu ni jambo ambalo limeanza kufanyika kwa wingi katika mitandao ya Kijamii na kwa hivyo kuna haja ya kulifanyia utafiti. Makala hii ina malengo matatu: kutoa mifano ya jumbe za mimu zinazoundwa na Wakenya katika mitandao ya Facebook na Whatsapp; kubainisha sifa za jumbe hizo kimuundo na kimtindo; na kuchunguza dhima ya utanzu wa mimu katika jamii. Mbinu ya utafiti iliyotumika katika kazi hii ni usanifu taaradhi na data ilichanganuliwa kwa kutumia Uchanganuzi maudhui ambapo data ilitambulishwa kwa kuiweka katika kategoria maalum. Mimu 51 zilizorejerelewa katika makala hii zilikusanywa kupitia kwa makundi ya Whatsapp anayoshiriki mwandishi na katika kurasa za Facebook za mtafiti na "˜marafiki' wake wa mtandaoni pamoja na kurasa za wasanii mashuhuri wa mimu. Mimu zilizorejelewa katika makala hii ziliundwa kati ya mwaka 2017 na 2021.Mimu hizo zimechanganuliwa kiisimu kwa kurejelea mawazo ya nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Kilongo ya Fairclough (1995). Nadharia hii imeafiki Uchanganuzi wa data husika na imefaulu katika kudhihirisha sifa na miundo ya mimu. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa mimu zinazoundwa na Wakenya huwa na dhima maalum katika jamii na pia huwa na sifa za kipekee kimuundo, kimsamiati, kisemantiki na kipragmatiki.
Keywords: Mimu; Usemi; Matini; Uchanganuzi Hakiki wa Kilongo; Diskosi (search for similar items in EconPapers)
Date: 2022
References: Add references at CitEc
Citations:
Downloads: (external link)
https://iprjb.org/journals/index.php/IJL/article/view/1632 (application/pdf)
Related works:
This item may be available elsewhere in EconPapers: Search for items with the same title.
Export reference: BibTeX
RIS (EndNote, ProCite, RefMan)
HTML/Text
Persistent link: https://EconPapers.repec.org/RePEc:bdu:ojtijl:v:3:y:2022:i:1:p:30-49:id:1632
Access Statistics for this article
More articles in International Journal of Linguistics from IPRJB
Bibliographic data for series maintained by Chief Editor ().