EconPapers    
Economics at your fingertips  
 

Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili

Mutisya Cosmas Mbithi (), Dr. Sarah Ndanu Ngesu () and Dr. Esther N. Chomba ()

European Journal of Linguistics, 2025, vol. 4, issue 2, 1 - 17

Abstract: Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia. Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2017). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini usahihi uhawilishaji huo. Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata. Uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera: Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.

Keywords: Viwakilishi vya kijinsia; Usahihi wa uhawilishaji; Tafsiri; Lugha lengwa; Hadharia lengwa. (search for similar items in EconPapers)
Date: 2025
References: Add references at CitEc
Citations:

Downloads: (external link)
https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/2783 (application/pdf)

Related works:
This item may be available elsewhere in EconPapers: Search for items with the same title.

Export reference: BibTeX RIS (EndNote, ProCite, RefMan) HTML/Text

Persistent link: https://EconPapers.repec.org/RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:1-17:id:2783

Access Statistics for this article

More articles in European Journal of Linguistics from CARI Journals Limited
Bibliographic data for series maintained by Chief Editor ().

 
Page updated 2025-06-12
Handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:1-17:id:2783