EconPapers    
Economics at your fingertips  
 

Usawiri wa Wahusika wa Kiume katika Riwaya ya Chozi La Heri

Agnes Mwongeli Kiema (), Dr. John Mutua () and Dr. Sarah Ndanu Ngesu ()

European Journal of Linguistics, 2025, vol. 4, issue 2, 41 - 48

Abstract: Makala hii imechunguza, usawiri wa wahusika wa kume katika riwaya ya Chozi la Heri (2017). Katika ulimwengu wa riwaya ya Kiswahili na fasihi, imekuwa kama jambo la kawaida kuona watafiti wengi wakichunguza masuala ya wanawake zaidi kuliko masuala ya wanaume. Jambo hili limetokana na ukweli kwamba, wanawake wamekuwa wakipiganiwa haki zao ili kuwafanya sawa na wanaume katika nyanja mbalimbali za maisha. Atieno (2019) anaeleza kuwa, kupuuzwa kwa jinsia ya kiume kumechangia hali yao ya upweke, kwani hakuna anayewafikiria wala kuwatetea kama inavyofanyiwa jinsia ya kike. Riwaya hii imeteuliwa kimakusudi kwa sababu inamsawiri mhusika wa kiume katika nyanja mbalimbali za maisha. Makala hii iliogozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inatakiwa kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo riwaya ya Chozi la Heri ilisomwa na kuhakikiwa. Ni matumaini yetu kuwa, Makala hii imetoa mwanga mkubwa kuhusiana na masuala ya jinsia ya kiume. Aidha, Makala hii itakuwa kichocheo cha watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume.

Keywords: Usawiri; Wahusika; Uhalisia; Jinsia; Nadharia; Fasihi. (search for similar items in EconPapers)
Date: 2025
References: Add references at CitEc
Citations:

Downloads: (external link)
https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/2879 (application/pdf)

Related works:
This item may be available elsewhere in EconPapers: Search for items with the same title.

Export reference: BibTeX RIS (EndNote, ProCite, RefMan) HTML/Text

Persistent link: https://EconPapers.repec.org/RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:41-48:id:2879

Access Statistics for this article

More articles in European Journal of Linguistics from CARI Journals Limited
Bibliographic data for series maintained by Chief Editor ().

 
Page updated 2025-08-18
Handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:41-48:id:2879