EconPapers    
Economics at your fingertips  
 

Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili

Dorcas Kasiva Kimondiu (), Dr. Francis Musyoka () and Dr. Esther Chomba ()

European Journal of Linguistics, 2025, vol. 4, issue 2, 49 - 67

Abstract: Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema (1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu za Jadi, (2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi. Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya. Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002). Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule. Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume. Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya. Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja. Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini.

Keywords: Usawiri; Wahusika; Uchanganuzu; Ulinganishi; Mtazamo (search for similar items in EconPapers)
Date: 2025
References: Add references at CitEc
Citations:

Downloads: (external link)
https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/2936 (application/pdf)

Related works:
This item may be available elsewhere in EconPapers: Search for items with the same title.

Export reference: BibTeX RIS (EndNote, ProCite, RefMan) HTML/Text

Persistent link: https://EconPapers.repec.org/RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:49-67:id:2936

Access Statistics for this article

More articles in European Journal of Linguistics from CARI Journals Limited
Bibliographic data for series maintained by Chief Editor ().

 
Page updated 2025-08-18
Handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:49-67:id:2936